Kuhusiana na tuhumu zao dhidi ya Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz na kwamba ni kibaraka cha serikali na mimi mwenyewe nimesikia jinsi wanavosema kwamba ni mwanaume mwanachuoni wa serikali, maneno kama hayo yanatoka tu kwa mtu Hizbiy pasi na kujali kama atakuwa ni katika Hizbiyyuun kama al-Ikhwaan al-Muslimuun au Hizbiyyuun wenye kujificha kama jumuiya ya al-Hikmah, al-Ihsaan, al-Iswlaah, baadhi ya wanachama wa jumuiya ya Ihyaa´ at-Turaath au Suruuriyyuun.

Ninataka mumdurusu mtu anayetamka maneno kama hayo. Utakuta ima ni katika Hizbiyyuun, mjinga (na hivyo ni mpumbavu mdogo) au mtu wa Bid´ah katika Shiy´ah na Suufiyyah.

Shaykh Ibn Baaz ni mmoja katika wanachuoni. Wakati mwingine anapatia na wakati mwingine anakosea. Wakati fulani anajua na wakati mwingine hajui. Wakati fulani anasahau. Wakati fulani ni mlaini kwa wanachuoni. Lakini ni wachache walio kama yeye. Ikiwa atatoa Fatwa yenye makosa pamoja na hivyo ana uzowefu. Ni mtumzima mwenye zaidi ya miaka sabini. Ana uzowefu wa mambo. Anajua kuwa uasi dhidi ya mtawala unapelekea tu katika shari.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 26/08/2020