Swali: Ni yapi maoni yako juu ya sifa ya kundi lililookoka, Firqat-un-Naajiyah? N kina nani? Ni upi mfumo wao? Ni ipi nchi yao ikiwa kama hilo limetajwa katika Hadiyth au maneno ya wanachuoni?

Jibu: Kundi lililookoka ni lile liliyoko katika mfano wa yale aliyokuwemo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifasiri hivyo. Mfumo wao ni kuwa wanafuata Qur-aan na Sunnah. Hawana mji maalum.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/159)
  • Imechapishwa: 24/08/2020