Swali: Nimeijua Hadiyth hii tangu kitambo na naifanyia bidii iliyokuwa kubwa, nayo ni hii ifuatayo:

“Ummah wangu utafarikiana katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu. Nalo ni lile lenye kufuata yale niliyomo mimi na Maswahabah zangu.”

Hadiyth hii siku zote niliijua hivi. Lakini hata hivyo nilikuwa nasoma baadhi ya vitabu na nikaona Hadiyth hii ikiwa na nyongeza yenye kusema:

“Yote yataingia Peponi isopokuwa moja tu.”

Ninaapa kwa Allaah ya kwamba upokezi huu umenitatiza sana. Uhalisia wa mambo ni kwamba yote yataingia Motoni isipokuwa moja au yote yataingia Peponi isipokuwa moja tu?

Jibu: Matamshi yaliyothibiti katika upokezi wote uliokuja ni:

“Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.”

Kuhusu upokezi wenye kusema:

“Yote yataingia Peponi isopokuwa moja tu.”

hauna asli yoyote.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/160)
  • Imechapishwa: 24/08/2020