Fawziy al-Bahrayniy amesema:
“Rabiy´ al-Madkhaliy amesema katika “al-Majmuu´ al-Waadhwih”[1]: “Njia ya kumi: “Wanaenda hatua kwa hatua kwa vitimbi kama wanavofanya Baatwiniyyah. Sisemi kuwa wao ni Baatwiniyyah, lakini wanafanana nao katika kwenda kwao hatua kwa hatua na kubadilishabadilisha rangi.”[2]
Ametaamiliana na maandiko haya kwa njia yake ya kizushi; anaficha yale aliyomo na kudhihirisha yale anayoamini yeye na kipote chake. Ni kweli kwamba niliyasema aliyoyataja na nikataja dalili juu ya maneno yangu. Nikasema baada yake:
“Hivi punde walikuwa wakijidhihirisha kuwaheshimu wanazuoni na kusema kwamba anayepingana nao basi amekadhibisha Uislamu, Qur-aan na Sunnah na kuubomoa Uislamu. Wanalingania wanazuoni wafuatwe kichwa mchunga kwa hamasa. Walipofikiri kuwa wameshapata nguvu na kukua, ndipo wakaanza kuwapiga vita hadharani, kuyatia upumbavuni maoni yao na wakawachochea wakorofi dhidi yao. Namna hii ndivo wanaenda hatua kwa hatua katika ulinganizi wao wa kisiri. Kwanza huanza kwa kudhihirisha kumuheshimu Imaam Ibn Baaz na Ibn Taymiyyah. Kisha huanza kuwadanganya taratibu mpaka pale wanapokuwa na uhakika kuwa wamewadhibiti. Basi hapo ndipo huanza kuwaangusha wanazuoni kwa njia yao ya vitimbi, mmoja baada ya mwingine mpaka wanapofikia kwa Ibn Taymiyyah.”
Isitoshe wanafanana na Raafidhwah. Pindi Raafidhwah wanapoogopa basi hujidhihirisha kuwaheshimu na kuwapenda Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na kuwaombea kwa Allaah awawie radhi. Pale tu wanapohisi amani basi huanza kuwatukana na kuwaponda. Haddaadiyyah hawa hufanya vivyo hivyo. Wanapohisi amani basi huanza kuwatukana wanazuoni. Tazama walivofanya kwa al-Albaaniy. Mwanzoni walijidhihirisha kumuheshimu, kumtetea na kuwatuhumu wale wote wanaomtuhumu Irjaa´ kwamba ni katika Khawaarij. Kisha baadaye wao wenyewe tena wakaanza kumtukana na kumtuhumu Irjaa´ na kupinda kutokana na mfumo wa Salaf.”[3]
[1] uk. 485.
[2] ar-Ru´uud as-Swawaa´iqiyyah, uk. 16.
[3] al-Majmuu´ al-Waadhwih, uk. 485-486.
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 48-49
- Imechapishwa: 24/09/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket