Hapa ndipo unaweza kusoma vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah

Swali: Wanafunzi wengi wanasema kuwa haki inachukuliwa kutoka kwa kila mtu hata mzushi. Hivyo inafaa kusoma vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah na kusikiliza darsa zao…

Jibu: Haijuzu kusoma vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah wala kusikiliza kaseti zao isipokuwa kwa lengo la kubainisha upotofu walionao ili uweze kuepukwa. Ama kusoma tu kawaida kitu ambacho kina madhara, ni jambo linalotakiwa kuepukwa. Badala yake anatakiwa kujishughulisha na kitu cha uhakika. Kuna mengi yenye amani na usalama ambayo mtu anaweza kusoma. Aachane na watu wenye kutia mashaka, wamepinda, makosa na kuteleza. Ajishughulishe na maneno yaliyo salama na asisemi kuwa anachukia haki yake na kuacha batili yake. Umri wako haukutoshi kusoma kila kitu na kusikiliza kila kitu. Kwa ajili hiyo jishughulishe na yale yaliyochujwa na yaliyohakikishwa. Mtu anaweza kusikiliza darsa fulani au akasoma baadhi ya vitabu ambapo akadhurika. Mambo kama hayo yanatakiwa kuepukwa. Ni kosa kusoma kitabu kujengea kwamba unachukua jambo fulani na kuacha lingine. Soma kitabu ambacho utachukua na kukubali kila kitu.

Mzungumzaji: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Marejeo: https://youtu.be/LfdUsxrdhgI
Tarjama: Firqatunnajia.com