5 – Kuchomoza kwa jua kutoka upande wa magharibi kwenda upande wa mashariki ni jambo limethibiti kwa Qur-aan na Sunnah. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَوْمَ يَأْتِي بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا

“Siku zitakapokuja baadhi za alama za Mola wako haitoifaa nafsi imani yake, ikiwa haikuamini kabla au haikuchuma katika imani yake kheri yoyote.”[1]

Makusudio yake ni kuchomoza kwa jua kutoka upande wa magharibi.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Qiyaamah hakitosimama mpaka lichomoze jua kutoka upande wake wa magharibi. Litakapochomoza basi watu wote wataamini. Na hapo ni pale ambapo:

لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا

“… haitoifaa nafsi imani yake, ikiwa haikuamini kabla au haikuchuma katika imani yake kheri yoyote.”

Kuna maafikiano juu yake[2].

[1] 06:158

[2] al-Bukhaariy (158, 4636) na Muslim (248, 157).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 110-111
  • Imechapishwa: 28/11/2022