Swali: Mtu anakufuru akionelea kuwa dhambi fulani ni halali? Je, madhambi yanatofautiana inapokuja katika kuonelea kuwa ni halali?

Jibu: Inahusiana na kuhalalisha dhambi ambayo kuna maafikiano juu yake kuwa ni haramu. Zingatieni! Yule mwenye kuoenelea dhambi ambayo kuna makubaliano juu yake kuwa ni haramu anakufuru. Hata hivyo hakufurishwi yule mwenye kuonelea kwua dhambi fulani ni halali ambayo hakuna maafikiano juu yake. Pamoja na hivyo anazingatiwa kuwa amekosea. Akumbushwe na kuzinduliwa kuwa kauli hii ni kosa na dalili inasema kinyume chake. Abainishiwe hili. Lakini asikufurishwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir-14340205.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015