Swali: Je, Bahaa-iyyah Bid´ah yao ni ya kufuru?

Jibu: Bila ya shaka. Bahaa-iyyah ni wale wanaidai kuwa Allaah Ameingia katika viumbe – Ametakasika Allaah na yale wanayoyasema. Bahaa-iyyah wanaonelea kuwa Allaah ameingia katika baadhi ya waja Wake. Huluuliyyah wao wanaonelea kuwa Allaah yuko kila mahali na hayuko juu mbinguni na wala hakulingana juu ya ´Arshi. Wanaonelea kuwa yuko kila mahali. Hawa ni Huluuliyyah kwa kuwa wanaonelea kuwa Allaah ameingia katika kila kitu – Ametakasika Allaah na yale wanayoyasema.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir-14340205.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015