Hapa ndipo mwanafunzi atahesabika ni mwanafunzi wa mwanachuoni

Swali: Mwanafunzi akisoma kitabu kwa mwanachuoni anahesabika kuwa ni mwalimu wake kwa sababu amesoma kwake kitabu fulani na anazingatiwa kama mmoja katika wanafunzi zake?

Jibu: Ndio. Akikaa kwake na akastafidi kutoka kwake na akahifadhi sehemu katika elimu, kunasemwa kuwa ni mwalimu wake katika kadhaa na kadhaa. Ni mwalimu wake katika Nahuw, Tafsiyr, Fiqh na kadhalika kwa kiasi na atakavyokuwa amejifunza kwake. Mtu anaweza kuwa na waalimu wengi. Anaweza kuwa na maelfu ya waalimu au mamia ya waalimu kama ilivyo katika historia ya wanachuoni na jinsi walivochukua elimu kwa waalimu.

Hii ni dalili inayoonesha katika elimu mtu asikomeke na fani moja tu. Asitosheke na kusoma fani ya Hadiyth tu. Elimu ni yenye kushabihiana. Baadhi inaitumikia nyingine. Ni lazima asome fani ya Tafsiyr, Hadiyth, Nahuw, lugha ya kiarabu, Usuwl-ul-Fiqh, Usuwl-ut-Tafsiyr na somo la Hadiyth. Asikomeke na fani moja na kusema inatosheleza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15243
  • Imechapishwa: 21/04/2015