Swali: Dada huyu anauliza hukumu ya Qur-aan inayoandikwa na kutundikwa nyumbani au kuvaliwa ikawa kama ni Hijaab?

Jibu: Hili halijuzu. Haijuzu kutundika Qur-aan kwa njia ya Hijaab. Hili limekatazwa na Salaf. Kauli sahihi ya wanachuoni ni kwamba haijuzu. Hata kama ni Qur-aan mtu asiitundike. Hata hivyo anaweza kusomewa Qur-aan. Hili ni jambo zuri. Ama kuhusu kuitundika haijuzu hata kama itakuwa ni Qur-aan.

Ama ikiwa [kilichoandikwa] ni kitu kingine mbali na Qur-aan, kama ushirikina na mambo ya uchawi, hili kwa makubaliano ni kwamba haijuzu. Ni hirizi za kishirikina. Vinavyotundikwa au kuvaliwa vimegawanyika aina mbili:

1- Qur-aan. Hili lina tofauti. Kauli sahihi ni kuwa haijuzu.

2- Mambo ya ushirikina na ya uchawi na matamshi ya kiajabu yasiyofahamika. Hili ni haramu kwa makubaliano. Ni Shirki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15243
  • Imechapishwa: 21/04/2015