Hakuna Ahl-us-Sunnah yeyote aliyepinga kuonekana kwa Allaah siku ya Qiyaamah

Swali: Kutofautiana baadhi katika masuala ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuona Mola Wake kama ilikuwa kwa macho au kwa moyo wake ni dalili inayoonesha kuwa Maswahabah walitofautiana katika ´Aqiydah?

Jibu: Hapana. Hawakutofautiana katika ´Aqiydah. Walitofautiana katika masuala maalum. Ama ´Aqiydah kuhusu kwamba Allaah Ataonekana siku ya Qiyaamah hawakutofautiana. Waislamu watamuona kwa macho yao. Je, kuna yeyote katika Ahl-us-Sunnah aliyepinga hili? Hakuna aliyepinga hili. Walichotofautiana ni kama alimuona kabla ya kufa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam), wakati alipokuwa bado yuhai, kwa sababu hakuna yeyote atayemuona Allaah duniani. Hakuna yeyote atayemuona Allaah duniani. Hakuna yeyote anayeweza kumuona Allaah duniani. Hili ni hata kwa Muusa (´alayhis-Salaam):

قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا

”Akasema: “Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” Akasema: “Hutoniona! Lakini tazama jabali, likitulia mahali pake, basi utaniona.” Basi Mola wako alipojidhihirisha katika jabali, alilijaalia kuwa lenye kupasukapasuka.” (07:143)

Jibali lilivurugika na likawa chenga chenga kutokana na ukubwa wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hakuna yeyote anayeweza kumuona Allaah duniani. Kuhusu Aakhirah Allaah Atawapa nguvu na Atawakirimu wamuone ili macho yao yaweze kuburudika. Wale waliomuamini duniani ilihali hawajamuona, Allaah (Jalla wa ´Alaa) atawakirimu siku ya Qiyaamah waweze kumuona kwa macho yao ikiwa ni ikram kwao. Ama makafiri ambao walimkanusha Allaah, Allaah atawazuia wasimuone siku ya Qiyaamah:

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ

“Hapana! Hakika wao siku hiyo watawekewa kizuizi [wasimuone] Mola wao.” (83:15)

Kwa kuwa hawakumuamini Allaah (´Azza wa Jall) duniani. Hivyo Allaah atawazuia wasimuone na atawanyima Pepo Yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/hadis-fitan-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015