Hapa ndipo itafaa kuhamisha zakaah kwenda mji mwingine

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… itachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupewa masikini wao.”

Hapa si inafahamisha kuwa haitakiwi kutolewa nje ya nchi hiyo?

Jibu: Wanakusudiwa mafukara wote. Hata hivyo bora zaidi ni watu wa mji huohuo. Mafukara wake ndio aula zaidi wakihitaji. Kama Allaah amewatajirisha basi itahamishwa kwenda miji mingine. Lakini watu wa maji huohuo ndio wana haki zaidi ya kupewa zakaah hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22768/ما-حكم-اخراج-الزكاة-الى-بلد-اخر
  • Imechapishwa: 19/08/2023