Anadai kuwa zakaah anapewa Mtume pekee

Swali: Mwenye kusema kuwa zakaah anapewa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake si anakuwa mwenye kupindisha maana?

Jibu: Afunzwe. Akiendelea apigwe vita. Allaah akimwongoza zakaah itachukuliwa kutoka kwake na ataadhibiwa kwa pesa. Kama ilivyokuja katika Hadiyth ya Bahz bin Hakiym:

“Naichukua na nusu ya mali yake hali ya kuwa ni haki katika haki za Mola wetu.”

Lakini wakipigana vita basi wapigwe vita kama walivofanywa wale walioritadi. Walipambana Abu Bakr as-Swiddiyq akawapiga vita. Lakini wasipopigana vita na wakaweza kuwalazimisha watalazimishwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22767/حكم-زعم-ان-الزكاة-لا-تودى-الا-للنبي-ﷺ
  • Imechapishwa: 19/08/2023