Hapa ndipo dhambi ya ndevu inakuwa kubwa

Swali: Mwenye kunyoa ndevu ni fasiki? Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma yake?

Jibu: Kunyoa ndevu ni haramu. Lakini hata hivyo sio dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa. Ni katika dhambi miongoni mwa madhambi yaliyo chini ya madhambi makubwa. Isipokuwa ikiwa kama atafanya hilo kwa kuendelea na akasema kuwa ni sawa na inajuzu, hapa ndipo itakuwa dhambi kubwa – tunaomba Allaah atukinge.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13958
  • Imechapishwa: 24/06/2020