al-Fawzaan mwanamme kufunika kichwa katika swalah

Swali: Mwenye kuswali kichwa wazi swalah yake ni pungufu? Je, Maswahabah walikuwa wakifunika vichwa vyao wakati wa kuswali?

Jibu: Kufunika kichwa ni katika ukamilifu:

خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ

“Chukueni mapambo yenu katika kila swalah.” (07:31)

Pambo la wajibu ni kufunika ´Awrah. Chenye kuzidi hapo kimependekezwa. Kila ambavyo mtu atajipamba imependekezwa. Miongoni mwa hayo ni mwanaume kufunika kichwa chake. Ni jambo limependekezwa kwa kuwa ni katika ukamilifu na kujipamba.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13958
  • Imechapishwa: 24/06/2020