Hapa ndio itafaa kutoa mali yote

Swali: Vipi mtu ataoanisha kati ya Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) kitendo chake cha kutoa mali yake yote na makatazo ya kutoa vyote na baada ya hapo mtu akawaomba-omba watu?

Jibu: Ikiwa mtu ana imani yenye nguvu kwa Allaah kama aliokuwa nayo Abu Bakr as-Swiddiyq, haina neno. Ama ikiwa mtu ana imani dhaifu na anahitaji kubakia na sehemu katika mali yake, anaweza kufanya hivo [kubaki na sehemu katika mali yake] kutokana na haja yake. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomuuliza alichoacha nyumbani kwa wanafamilia yake, akasema:

“Nimemwacha Allaah na Mtume Wake.”

Hii inaonyesha nguvu ya imani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2025-12-1435.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015