Swali: Kuna watu wanaojiita “walaji mboga”. Wanakula mbogamboga tu…

Jibu: Hawa ndio ambao Ibn-ul-Qayyim ametaja hapa! Wanakula tu mbogamboga kwa kuwa hakuna haramu yoyote ndani yake, haikufungamana na ribaa… Huku ni kuipa nyongo dunia kuliko kubaya.

Swali: Je, huku kunazingatiwa ni kuharamisha halali?

Jibu: Ndio. Hii ni aina ya kuharamisha halali. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا

“Kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu.” (07:31)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ

“Enyi mlioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye Pekee.” (02:172)

يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ

“Enyi watu! Kuleni katika vilivyomo ardhini vya halali, vizuri na wala msifuate nyayo za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.” (02:168)

Allaah ametuhalalishia vizuri na ametuharamishia vilivyo vichafu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2025-12-1435.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015