Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kuwapa hongera makafiri kwa sikukuu zao?

Jibu: Haijuzu kufanya hivi kwa kuwa huku ni kuwashaji´isha na njia ya kuonesha furaha kwa Bid´ah na furaha zao. Isipokuwa tu wakati wa dharurah. Hili linaweza kufanywa na mfano wa mtawala. Anawapa hongera kisiasa kwa kuepuka shari yao na sio kwa kukubaliana na dini yao. Hili linaweza kuwa linajuzu kwa mtawala peke yake. Ama kwa Waislamu wote haijuzu kuwapa hongera makafiri:

وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا بِاللَّغْوِ مَرُّوا كِرَامًا

“Wale ambao hawashuhudii uongo na wanapopita kwenye upuuzi hupita kwa heshima.” (25:72)

Bi maana hawashuhudii sikukuu za makafiri. Makusudio ya (الزُّور) hapa ni sikukuu za makafiri. Hawahudhurii kwayo wala hawawapi hongera wake wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/nawaqid-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2015