Hammaad al-Answaariy kuhusu Saudi Arabia

Tunapokuja katika kulinganisha Asia na Afrika, ukweli wa mambo ni kwamba elimu Asia haikuwa kama ilivyokuwa baada ya kuasisiwa nchi hii. Kwa sababu nchi hii – nchi ya mfalme ´Abdul-´Aziyz – imekuja kwa kheri nyingi khaswa Asia na ulimwenguni kote kwa jumla. Kabla ya nchi hii wanazuoni hawakuwa wakiitilia umuhimu Tawhiyd Asia kama inavyotakikana. Wala hawakuwa wakitilia umuhimu Hadiyth kama inavyotakikana kufanyiwa kazi. Ulikuwa unaweza kupata baadhi ya wanazuoni Asia wanajishughulisha Hadiyth, lakini hawazifanyii kazi. Wanaegemea tu yale yanayoafikiana na madhehebu yao. Vilevile hawakuwa wakitilia umuhimu wasifu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama inavyotakikana. Lakini kwa tawfiyq ya Allaah (´Azza wa Jall) wakati ilipokuja Saudi Arabia, ambayo tunataraji kuwa ndio kundi lililookoka, ilikuja na kazi kubwa. Nchi hii iliuzindua ulimwengu wa Kiislamu kwamba ni lazima kuwepo suala la elimu na ikite zaidi katika mambo mawili:

1 – ´Aqiydah, ambayo ndio msingi.

2 – Qur-aan na Sunnah vinapaswa kufanyiwa kazi na sio kuvisoma peke yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Hammaad bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Majmuu´ (2/826)
  • Imechapishwa: 28/03/2024