´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh kuhusu Saudi Arabia

Tangu kuasisiwa kwa Saudi Arabia zaidi ya karne mbili zilizopita – na himdi zote anastahiki Allaah – ni nchi ya Salafiyyah inayohukumu kwa Shari´ah ya Allaah. Imeendelea kuwa imara juu ya hilo kwa msaada wa Allaah (Subhaanah). Bado ni yenye kuendelea juu ya mfumo huohuo na himdi zote anastahiki Allaah. Allaah kwayo ameunufaisha Uislamu na waislamu katika nyanja nyingi. Inapokuja katika elimu imeeneza ya Shari´ah na ambayo ni sahihi. Vivyo hivyo imelingania kwa Allaah ulimwenguni kote. Imeeneza vitabu na khaswa Kitabu cha Allaah (Subhaanah).

Jengine ni kwamba inatilia umuhimu mahitaji ya waislamu katika kila mahali. Inahakikisha kuyanusuru mambo mbalimbali yanayohusu ummah. Haya ni mambo yenye kuenea na wanayashuhudia maadui na marafiki.

Aidha inatia bidii kubwa katika kuihudumia misikiti miwili Mitukufu na kufanya wepesi njia za Hajj na ´Umrah. Isitoshe inajenga misikiti na vituo vya Kiislamu ulimwenguni kote na mengi mengine.

  • Mhusika: ´Allaamaah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Gazeti ar-Riyaadh (12175)
  • Imechapishwa: 28/03/2024