Saudi Arabia ni ufalme wa Kiislamu na himdi zote njema anastahiki Allaah. Nchi inahukumu kwa nidhamu na Shari´ah ya Kiislamu. Misingi ya kazi yake na mifumo yake imepangwa kwa njia ya kutoenda kinyume na Uislamu. Wakati nchi inapopinga kitendo kama hicho[1] inafanya hivo kutokana na mpangilio wa dini yake, kwa sababu ndio nchi ambayo ipo misikiti miwili Mitukufu na chimbuko la ujumbe. Kwa hiyo haishangazi kwamba inakaripia machafu, kuchukia uhalifu wa wahalifu na kumtahadharisha kila ambaye anafanya uhalifu au anaridhia uhalifu wake.

[1] Shaykh Abu ´Umar Usaamah bin ´Atwaa’ bin Hamad amesema: ”Anakusudia shambulio dhidi ya WWC New York.”

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujj al-Qawiyyah ´alaa Wujuub-id-Difaa´ ´an-id-Dawlah as-Su´uudiyyah, uk. 108
  • Imechapishwa: 28/03/2024