Mambo yangelikuwa vipi kama talaka ingelikuwa mkononi mwa mwanamke? Mizani ingelivurugika na maisha ya kindoa yasingelikuwa na utulivu. Hilo ni kutokana na kule kuathirika haraka kwa mwanamke, kusukumwa kwake na hisia na udhaifu wake. Kwa sababu hakuna kinachomsukuma kufanya subira na kuvumilia, kwani hakuna chochote kinachomgarimu. Yeye ni mwenye kuletewa pesa.

Jengine ni kwa sababu pengine akapendezwa na mwanaume mwingine na hivyo ikampelekea kutoa talaka na kuondoka zake na kuolewa na aliyemtamani na kumpenda. Allaah ni Mjuzi wa kila kitu na Mwenye hekima juu ya viumbe Wake.

Tunaingia ndani ya mada yetu, nayo ni sababu za talaka. Huenda tusiweze kuziwekea kikomo sababu za talaka. Tunasema yafuatayo:

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 19
  • Imechapishwa: 28/03/2024