Hali ya wengi wanaowatibu watu hii leo

Swali: Kuna mtu yuko na jini linamuhudumia na anawatibu watu. Wanawake wanapomwendea anawaelekeza katika habasoda, asali na dawa nyingine za kiarabu na kiislamu. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Haina neno ikiwa anawaeleza watu kuwa hajui ghaibu, hanufaishi na wala hadhuru badala ya Allaah. Katika hali hiyo ni mkweli katika anayoyasema. Lakini ikiwa anaogopa pindi anapojiliwa na wanaolingania kwa Allaah na anajidai kuwa anatibu kwa asali, habasoda n.k. ilihali ukweli wa mambo anatibu kwa uchawi, huyo ni kuhani.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 18/01/2025