Swali: Baadhi ya wanafunzi wanasema kuwa mashairi ya al-Buwswayriy[1] wamesomwa na Salaf na maana yake ni sahihi.

Jibu: Haya sio maneno mazuri. Haya ni maneno batili. al-Burdah ni shirki. Ni kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jall) kuliko wazi. Hakuna anayeyatetea isipokuwa ima ni mjinga au mpotevu anayeikubali batili na shirki.

Swali: Je, mtu afaidike nayo kwa njia ya balagha na lugha?

Jibu: Asifaidike nayo. Ni batili. Ndani yake hakuna balagha wala lugha yoyote. Kama unataka balagha na lugha soma mashairi yenye msingi kama vile “al-Mu´alaqaat-us-Sabiy´” na mashairi na washairi kabla ya kuja Uislamu ambao walikuwa na ufaswaha, balagha na lugha. Kuhusu bwana huyu sio mwanachuoni wa lugha wala mwanachuoni wa balagha. Bwana huyu alikuwa ni khurafi ambaye alisoma mashairi haya ya shirki, ya kizushi na ya kichupa mipaka. Hayana maana yoyote. Ni wajibu kuyachana.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/145-shirki-katika-mashairi-ya-al-burdah/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
  • Imechapishwa: 18/02/2024