Hakika baadhi ya watu utawaona hawana kazi nyingine isipokuwa kumzungumza vibaya mtawala katika kila kikao wanachokaa, kukiuka heshima zao na kueneza makosa yao na huku wakifumbia macho yale mazuri yao na yale wanayopatia. Hapana shaka kwamba kupita mapito haya na kuvunja heshima za watawala hakuzidishi isipokuwa kuifanya hali kuwa mbaya zaidi. Kwani hakuondoshi tatizo na wala manung´uniko. Bali kunazidisha tu mabalaa. Aidha kunapelekea watawala kubughudhiwa, kuchukiwa na kutotekeleza amri zao ambazo zinapaswa kutiiwa.

Hatuna shaka kwamba watawala wanaweza kufanya vibaya na kukosea kama walivyo wanadamu wengine wote. Kwani hakila mwanadamu ni mwenye kukosea na mbora katika wakosefu ni yule mwenye kutubia. Hatuna shaka pia kwamba haijuzu kwetu kumnyamazia mtu yeyote ambaye ametenda kosa mpaka tufanye kile tunachoweza katika uwajibu wa kumnasihi kwa ajili ya Allaah, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na watu wa kawaida.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujj al-Qawiyyah ´alaa Wujuub-id-Difaa´ ´an-id-Dawlah as-Su´uudiyyah, uk. 46-47
  • Imechapishwa: 31/03/2024