Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, jamaa zake, Maswahabah zake na wale wote watakaofuata mwenendo wao.

Kutokana na maneno ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hamshukuru Allaah yule ambaye hawashukuru watu.”[1]

nawashukuru shukurani za dhati watawala wa nchi hii iliobarikiwa –  nchi yenye misikiti miwili Mitukufu ya Saudi Arabia – na khaswa mtumishi wa misikiti miwilii Mitukufu mfalme Salmaan bin ´Abdil-´Aziyz (Hafidhwahu Allaah), mrithi wake wa ufalme Muqrin bin ´Abdil-´Aziyz na waziri wa mambo ya ndani na naibu wake waziri mkuu wa mambo ya ndani Muhammad bin Naayif bin ´Abdil-´Aziyz – Allaah awahifadhi wote – na serikali yao salama kwa yale wanayosimama nayo katika kunusuru Uislamu na waislamu ni mamoja ndani na nje ya nchi, kueneza Tawhiyd na Sunnah na kuwaheshimu wanazuoni wa ummah. Nawashukuru pia kunifanyia wepesi kuingia ndani ya nchi kufanya matibabu katika hali hizi nzito na ngumu. Natanguliza shukurani zangu za kipekee kwa mtukufu na mwanamfalme Muhammad bin Naayif, mkuu wa Jiyzaan Muhammad bin Naaswir na mwanawe aliyebarikiwa Faysaal kwa kunisaidia kuanzia pale nilipoanza kuingia ndani ya nchi hii hadi hivi sasa. Nawashukuru pia ndugu zake na ndugu zake wengine wote waliotupokea na kutukirimu kwa hali hali ya juu kabisa. Nayasema haya kama wajibu wangu mbele ya Allaah na sio ajili ya kutaka kujipendekeza kwa yeyote. Nimelelewa katika nchi hii kwa miaka mingi juu ya Tawhiyd na Sunnah. Sisahau wema wake hivi sasa wakati nimelala juu ardhi yake na sijui kile ambacho Allaah ameniandikia katika siku zijazo.

Kadhalika nawashukuru wanazuoni wa nchi hii kwa yale waliyoyafanya na wanaendelea kuyafanya katika kueneza Tawhiyd, Sunnah na kupambana na shirki na Bid´ah katika nchi hii na nje yake. Faida zao zimeenea ulimwenguni kote. Allaah awarehemu wafu wao na awahifadhi wale walio hai. Namlenga zaidi Imaam ´Abdul-´Aziyz bin Baaz, ´Allaamah Ibn ´Uthaymiyn, Muftiy wa sasa Shaykh ´Abdul-´Aziyz Aalush-Shaykh, ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan na wengine wote katika baraza la al-Lajnah ad-Daaimah katika nchi hii iliyobarikiwa.

Siwasahau wanazuoni wa al-Madiynah na mashujaa wa Tawhiyd na Sunnah kama vile ´Allaamah ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad, ´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy, ´Allaamah Swaalih as-Suhaymiy na ´Allaamah Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Allaah awarehemu wale waliokufa na atukusanye pamoja na Mitume, wakweli, mashahidi na waja wema…

Imeandikwa na Abu Ibraahiym Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy al-´Abdaliy.

1436-07-01/2015-04-20

ar-Riyaadh

[1] Ahmad, Abu Daawuud na Ibn Hibbaan kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=152031
  • Imechapishwa: 31/03/2024