Swali: Je, anapewa udhuru kwa ujinga anayemtukana Swahabah kwa kutokujua? Je, anakuwa kafiri?
Jibu: Ni mjinga? Vipi atakuwa hajui jambo hili? Ni vipi atamtukana Swahabah kwa ujinga? Ni kipi asichojua? Hawajui Maswahabah? Hapa hakuna ujinga wowote. Mwenye kuwatukana Maswahabah ni zindiyq. Hapa hakuna ujinga wowote. Wengine wanamtukana Allaah [kwa madai ya ujinga] na huyu anawatukana Maswahabah na kusema ni mjinga. Vipi mtu ataweza kumtukana Allaah kwa ujinga au kufanya mzaha na Allaah kwa ujinga? Huyu ni mwenye kuritadi na hii sio nafasi ya ujinga. Huyu sio mjinga. Ujinga unakuwa katika mambo makubwa na yaliyojificha. Haya ni mambo yaliyo wazi. Huyu hakuwatukana isipokuwa ni kutokana na maradhi alionayo ndani ya nafsi yake.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4716
- Imechapishwa: 17/11/2014
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)