Haya ni maneno yanayosemwa na mtu asiyejua analolisema

Swali: Kuna wenye kusema kuwa yule anayeomba kaburi na kuwaita watu kwalo haitwi kuwa ni mshirikina, bali mtu anasema kuwa amefanya Shirki. Je, maneno haya ni sahihi kama jinsi yalivo?

Jibu: Hapana. Huyu ndio mshirkina. Mtu anasema kuwa amefanya Shirki na ni mshirikina. Hakuna tofauti kati yake. Hakuna tofauti kati ya kusema amefanya Shirki na ni mshirikina. Haya ni maneno yasiyokuwa na maana. Mwenye kuabudu kaburi na kuita kwalo, mtu anasema kuwa amefanya Shirki, ni mshirikina na anaabudu mungu asiyekuwa Allaah. Majina yote haya anapewa yeye. Vilevile mtu anasema kuwa ni kafiri na ameritadi. Haya ni maneno yanayosemwa na mtu asiyejua anachokisema.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4716
  • Imechapishwa: 17/11/2014