Hakuna kitu kipya kutoka kwa Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab

Swali: Siku mbili zilizopita umesema kuwa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab hakuna na jipya kwa sababu Wahhaabiyyah hayazingatiwi kuwa madhehebu. Je, mtu anaweza kusema kuwa madhehebu manne yameleta kitu kipya?

Jibu: Wamekuja na ijtihaad za ki-Fiqh, jambo ambalo wanalistahikia. Walikuwa wanastahiki kufanya ijtihaad zao na kunyofoa hukumu. Shaykh alilingania katika madhehebu ya Salaf  na katika Tawhiyd. Huku sio kunyofoa hukumu alikofanya au kitu ambacho yeye mwenyewe ndivo kafahamu. Ilikuwa ni mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake na Salaf. Kwa msemo mwingine yeye ni mfanya upya na muhuishaji wa yale mambo ya dini yaliyosahaulika au mbainishaji wa yale yaliyozuliwa ndani yake. Hana madhehebu yake mwenyewe. Madhehebu yake yeye ni madhehebu ya Hanaabilah. Yeye ni Hanbaliy katika Fiqh na ´Aqiydah yake ni ya Salaf. Madhehebu ya Salaf hayakufupika kwa Wahhaabiyyah – madhehebu ya Salaf ni ile ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika zama zote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (29)
  • Imechapishwa: 11/02/2022