Hakuna du´aa maalum ya sujudu ya kusahau

Swali: Kuna du´aa maalum inayosomwa baina ya Sujuud-us-Sahuw na katika Sujuud-us-Sahuw?

Jibu: Sujuud-us-Sahuw ni kama Sujuud ya swalah. Hapo anasema kama anavyosema katika Sujuud ya swalah:

سبحان ربي الأعلى

“Utakasifu ni wa Mola Wangu, Aliye juu.”

na aikariri. Sujuud-us-Sahuw haina du´aa maalum.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-10-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020