Swali: Adhaana ni lazima kwa anayeswali peke yake au pamoja na mkewe?

Jibu: Akiwa yuko katika mji adhaana ya msikitini inatosheleza. Na kama mtu yuko nchi kavu ni jambo limependekezwa.

Swali: Watu wanatakiwa kuwa wangapi ili ihesabike kuwa ni mkusanyiko?

Jibu: Chini chini wawe wawili. Hadiyth inasema:

“Chini chini watu wawili ndio mkusanyiko.”[1]

[1] Dhaifu sana kwa mujibu wa an-Nawawiy katika ”al-Khulaaswah” (2/674), dhaifu kwa mujibu wa Ibn-ul-Mulaqqin katika ”Ghaayat-ul-Ma’muul” (56) na ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Iswlaah-ul-Masaadjid”, uk. 51.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-10-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020