Swali: Je, kuna tofauti kati ya ´Aqiydah na manhaj?

Jibu: Hili swali limeshaulizwa sana na limeshajibiwa na Mashaykh wengi, nami pia nimeshalijibia. Niwezelo kusema ni kwamba, hizi ni katika kampeni za vipote vya kisiasa ambavyo wanadanganyika navyo vijana wa Salaf. Wanasema mfano wa upuuzi kama huu “Mimi niko katika ´Aqiydah ya Salaf, manhaj ya al-Ikhwaaniy [al-Muslimuun] au manhaj at-Tabliygh.” Haya ni maneno yanayotoa dalili tosha ya shari kwa mwenyenayo, fikira hii ya Kishaytwaan. Vipi utaigawa Dini katika mafungu mawili; ´Aqiydah na manhaj na kuchukua katika Dini yale nitakayo na kuacha yale nisiyotaka?

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ

“Haiwi kwa muumini mwanamme na wala kwa muumini mwanamke, anapokidhia Allaah na Mtume Wake amri yoyote ile iwe wana khiyari katika amri yao.” (33:36)

Vipi utachukua ´Aqiydah – kama unavyodai – na ukachukua manhaj ambayo inakhalifu manhaj ya Ahl-us-Sunna wa-Jamaa´ah? manhaj ambayo imejengeka kuipiga vita ´Aqiydah ambayo unajinasibisha kwayo ikiwa kweli wewe ni mkweli! Manhaj hii inayokhalifu manhaj ya Salaf lazima iwe inapigana vita na manhaj ya Salaf. Na wewe hapo ndio utakuwa askari katika manhaj hii, ukiisaidia kuipiga vita manhaj Salaf. Na hili nalisema kwa ujuzi. Tumeona watu sampuli hii, wanaodai kwamba wana ´Aqiydah ya Salafiyyah ilihali wako pamoja na al-Ikwaan [al-Muslimuun] au wengineo katika watu wa fitina wanaowapiga vita watu wenye ´Aqiydah na manhaj ya Salaf. Huu ni udanganyifu ambao wamedanganyika nao watu wengi.

Ahl-us-Sunnah wote wamekubaliana ya kwamba haijuzu mgawanyo huu kati ya ´Aqiydah na manhaj, hata tukisema ya kwamba kuna tofauti kati ya ´Aqiydah na manhaj [ya kimaana]. Kwa hakika, ni vitu viwili vinavyoenda sambamba kama ilivyo Shahaadatayn; ashhadu anlaa ilaaha illa Allaah, wa ashhadu anna Muhammad Rasuulu Allaah. Kwa hivyo haijuzu kuvigawa wala kuvitofautisha isipokuwa kwa mtu mpotofu. Na Ahl-us-Sunnah wamekubaliana kwa hili.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/catplay.php?catsmktba=355
  • Imechapishwa: 28/07/2020