Hakukamilisha Twawaaf ya kuaga kwa sababu ya kutoweza

Swali: Ni ipi hukumu mtu asipotimiza Twawaaf ya kuaga (طواف الوداع) kwa sababu ya kutoweza?

Jibu: Ni lazima kwake kuirudia maadamu bado yuko hapo. Ikiwa amesharejea kwao, basi atoe kafara ya kuchinjwa. Kwa sababu ameacha wajibu miongoni mwa mambo ya wajibu ya hajj, ambalo ni Twawaaf ya kuaga.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (39)
  • Imechapishwa: 01/06/2023