Swali: Ni ipi hukumu mwanaume akimtaliki mwanamke kisha baadaye akamrejea kupitia mikono ya mwanaume ambaye sio ndugu yake?
Jibu: Ikiwa eda haijamalizika basi haikuwekwa sharti amrejee kupitia mikono ya ndugu zake wala kupitia mikono ya mtu mwingine. Bali ashuhudishe:
وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ
“… na mshuhudishe mashahidi wawili wenye uadilifu katika nyinyi.”[1]
Asiposhuhudisha na akamrejea kwa njia kumjamii inafaa. Kwa mujibu wa maoni sahihi ni kwamba inapendeza kushuhudisha na sio jambo la lazima. Lakini ikiwa eda yake imemalizika au talaka kubwa, basi haifai kumuoa isipokuwa kupitia walii. Hivo ndivo ilivyokuja katika Sunan kupitia kwa Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh). Isipokuwa kama walii atampa jukumu hilo mtawala. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Walivutana, basi mtawala ni walii wa asiyekuwa na walii.”
Ikiwa mtawala hahukumu kwa haki, basi itafaa akateuliwa mwanaume muheshimiwa na akamfungisha ndoa.
[1] 65:02
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 444
- Imechapishwa: 15/07/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket