Swali: Ni ipi hukumu ya kusherehekea siku ya taifa na pia wiki ya Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab? Ikiwa si Bid´ah, basi kuna tofauti gani baina yake na Bid´ah?

Jibu: Kusherehekea siku ya taifa ni Bid´ah. Siku ya taifa ni Bid´ah. Ama wiki za wanazuoni, si Bid´ah. Wiki za wanazuoni si sherehe, bali ni maonyesho ya vitabu vyao. Maana yake ni kwamba katika wiki hizo huonyeshwa vitabu walivyoandika wanazuoni hao, vitabu vinavyouzwa na kufahamishwa watu yale waliyoyaandika na yaliyochapishwa. Ikiwa ikasemwa kwamba wiki ya kitabu fulani, wiki ya imamu fulani, wiki ya Shaykh-ul-Islaam, wiki ya al-´Izz bin ´Abdis-Salaam, wiki ya al-Qurtwubiy na mfano wa hao, basi hii si sherehe. Bali ni kuonyesha vitabu, kuviuza na kuvisambaza miongoni mwa watu. Hili si Bid´ah. Kuhusu siku ya taifa na kuisherehekea siku ya taifa au siku nyingine yoyote kwa sura ya sherehe na kusherehekea usiku wa Raghaaib, haya yote ni Bid´ah. Yote hayo ni Bid´ah na ni miongoni mwa kujifananisha na maadui wa Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2365/حكم-الاحتفال-باليوم-الوطني-والاسابيع-الدعوية
  • Imechapishwa: 09/01/2026