Ahl-ul-Bid´ah ndio wenye kuchupa mipaka

Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth isemayo:

”Wameangamia waliochupa mipaka.”

aliyoipokea Muslim?

Jibu: Hii ni Hadiyth Swahiyh. Ameipokea Muslim na wengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wameangamia waliochupa mipaka.”

Akairudia mara tatu.

Maana ya (التنطع) ni kujitakalifisha, kujitia katika mambo kwa kina kupita mipaka na kuzusha. Hii Hadiyth ni dalili miongoni mwa hoja za Ahl-us-Sunnah dhidi ya wazushi, kwa sababu ni wenye kujikakama na kujikalifisha. Mwenye kuchupa mipaka ni mwenye kujikalifisha na kujitia katika mambo kwa kina ambaye anauliza juu ya mambo na kufanya mambo ambayo hayakuweka Allaah katika Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2371/الحكم-على-حديث-هلك-المتنطعون
  • Imechapishwa: 09/01/2026