Swali: Inafaa mtu kutumia fursa ya kulingania watu katika Tawhiyd, Uislamu au Sunnah bila ya kukataza maasi yaliopo?

Jibu: Hapana, haijuzu. Haijuzu. Na hili ndo nililokuwa nakhofia. Na kwa nini asijumuishe baina ya mazuri mawili kwa wakati mmoja? Kwa nini asikatazi maasi ayaonayo mbele yake na wakati huo huo akalingania watu katika Tawhiyd? Kwa kuwa ananyamazia maovu na kufanya ni njia ya kulingania katika Tawhiyd. Njia hizi zinarudi katika njia zile za kwanza tulizozihadithia, kuwa haijuzu kutumia michezo kama njia ya kuwalingania watu katika Uislamu. Haijuzu pia kunyamazia madhambi yanayotendeka mbele yetu kwa kukataza maovu makubwa zaidi. Nia nzuri haifanya njia kujuzu. Utapokuwa baina ya maovu, ni lazima kuukataza khaswa pale ambapo maovu haya tunapata dalili yake katika vitabu hivi vilivyoandikwa na hawa Mashaykh ambao hawa watu wa Bid´ah wanawategemea. Sura hii haijuzu iliokuja katika swali la mwisho. Badala yake ni wajibu kukataza maovu wanayotumbukia humo na wakati huo huo kuwalingania katika Tawhiyd. Inapaswa kuwa hivi na Allaah (Ta´ala) anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawa Juddah (16 B)
  • Imechapishwa: 09/04/2022