Haijuzu kuhifadhi picha kwenye kifaa chochote

Swali: Kuhifadhi picha za viumbe wenye roho na picha zilizopigwa kwa njia ya simu kwenye simu hiyo hiyo kunaingia katika uharamu?

Jibu: Ndio, kunaingia katika uharamu. Kila kinachohifadhi picha na kukibakiza basi ni haramu; sawa ikiwa ni kwa njia ya simu, karatasi au ukuta. Vyote hivyo ni picha za haramu. Amelaaniwa mwenye kuyafanya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2138
  • Imechapishwa: 12/07/2020