al-Fawzaan kuhusu ujinga ni udhuru 17

Swali: Nikiona mtu anasujudia kaburi nimhukumu kusema kuwa ni mshirikina au ni lazima kwanza kumsimamishia hoja? Ni yapi makusudio ya kusimamisha hoja?

Jibu: Ikiwa mtu huyu anayesujudia kaburi ametengana na ulimwengu wa Kiislamu na hajafikiwa na Qur-aan wala Sunnah, huyu anazingatiwa kuwa ni mjinga. Hivyo anatakiwa kufunzwa na kubainishiwa. Asimamishiwe hoja. Ama ikiwa anaishi kati ya waislamu na isitoshe katika mji wa Kiislamu ambapo anasikia Qur-aan na huenda hata amehifadhi Qur-aan yote kwa visomo vyake kumi kisha anasujudia kaburi hana udhuru. Mtu huyu hana udhuru kwa kuwa amefikiwa na Qur-aan. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ

“Nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.” (06:19)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2136
  • Imechapishwa: 12/07/2020