Mume hataki mke ashike mimba ilihali mke yuwataka

Swali: Dada huyu anayetoka Ufaransa anauliza kwa kusema ya kwamba ana watoto wawili na anataka kuzaa watoto wengine, lakini hata hivyo mume wake anamkatalia. Hoja yake ni kwamba hawapatani naye na hajui kama wataendelea au wataachana. Anauliza kama inajuzu kubeba mimba bila idhini yake?

Jibu: Haijuzu kwake [mke] kumuitikia kuzuia mimba. Asimuitikie kukubali kuzuia mimba. Kwa kuwa haya ni maasi. Ushikaji mimba na kuzaa kizazi kingi ni kitu kinachotakikana. Asimuitikie katika hilo. Lau atashika mimba ni vizuri na ni kheri zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2138
  • Imechapishwa: 12/07/2020