Swali: Unapendekeza kwa mwanafunzi ahifadhi Zaad-ul-Mustaqni´ au ´Umdat-ul-Fiqh?

Jibu: Haihusiani na kuhifadhi. Kuhifadhi sio kujifunza hata kama utahifadhi al-Mughni´. Huku sio kujifunza. Inahusiana na kwamba ukipata mwalimu anayeweza kukufunza na kukushereheshea kitabu, kila siku ukawa unahifadhi sehemu yake na akakushereheshea nayo. Kwa msemo mwingine ukakusanya kati ya kuhifadhi na kujifunza. Hili ni jambo zuri. Lakini kukaa tu na kuhifadhi sio kujifunza hata kama ungehifadhi dunia nzima. Hii ni ghururi tu. Huenda ukapatwa na ghururi ya kujiona uko mwanachuoni ilihali uko mjinga ingawa umehifadhi. Elimu sio kuhifadhi. Elimu ni ule uelewa:

“Yule ambaye Allaah anamtakia kheri humpa uelewa katika dini.”[1]

Uelewa ni kule kufahamu. Hili ndilo linatakikana. Ni wangapi wamehifadhi vitabu na hawaelewi kitu! Ukimuuliza kitu kidogo tu hawezi kukujibu.

[1] al-Bukhaariy (71).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (6) http://alfawzan.af.org.sa/node/14379
  • Imechapishwa: 02/12/2016