Imaam an-Nawawiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

194 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

أفْضَلُ الجِهَادِ كَلِمَةُ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائرٍ

“Jihaad bora ni kusema neno la uadilifu mbele ya mtawala dhalimu.”[1]

Abu Daawuud na at-Tirmidhiy na amesema kuwa ni nzuri.

Kuna hali nne:

1 – Kutamka neno la haki mbele ya mtawala ambaye ni mwadilifu. Hii ni sahali.

2 – Kutamka neno la batili mbele ya mtawala mwadilifu. Hili ni khatari. Unaweza kumfitinisha mtawala mwadilifu kwa maneno yako kutokana na jinsi unavyompambia nayo.

3 – Kutamka neno la haki mbele ya mtawala mkandamizi. Hii hi jihaad bora.

4 – Kutamka neno la batili mbele ya mtawala mkandamizi. Hili ni baya zaidi na zaidi.

Hivi ni vigawanyo vinne. Lakini lililo bora kuliko yote ni kutamka neno la haki mbele ya mtawala dhalimu. Ninamuomba Allaah atujaalie kuwa miongoni mwa wale wenye kutamka haki kama haki na kwa kina juu ya nafsi zetu na kwa wengine.

[1]Abu Daawuud (4344) na at-Tirmidhiy (2174).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (2/454)
  • Imechapishwa: 21/08/2025