Haijuzu kwa mwanaume kuvaa pete ya dhahabu, cheni ya dhahabu, kuvaa nguo ilio na sehemu ya dhahabu na kadhalika. Ni wajibu kwa mwanaume ajiepushe na dhahabu zote. Dhahabu anaivaa anayehitajia uzuri na kujipamba, kama mwanamke. Anavaa ili ampambie mume wake ili avutikiwe naye. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
أَوَمَن يُنَشَّأُ فِي الْحِلْيَةِ وَهُوَ فِي الْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ
“Hivi kweli yule aliyelelewa katika mapambo naye katika mabishano si mbainifu.” (43:18)
Wanawake wanahitajia dhahabu ili kuwapambia waume. Mwanaume hahitajii hilo. Mwanaume anapambiwa nawala hajipambi kwa ajili ya mwingine. Isipokuwa baina yake yeye na mke wake kwa kila mmoja kumpambia mwenzake kutokana na mshikamano unaopatikana kwa kufanya hivo.
Lakini pasina kujali lengo wala hali yoyote ile haijuzu kwa mwanaume kuvaa dhahabu. Lakini kuvaa fedha ni sawa. Inajuzu kwa mwanaume kuvaa pete ya fedha. Lakini kwa sharti katika kufanya hivo kusiwepo imani fulani kama wanavofanya baadhi ya watu wanapowaiga manaswara katika kuvaa pete ya ndoa kati ya wanandoa.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (2/444-445)
- Imechapishwa: 21/08/2025
Haijuzu kwa mwanaume kuvaa pete ya dhahabu, cheni ya dhahabu, kuvaa nguo ilio na sehemu ya dhahabu na kadhalika. Ni wajibu kwa mwanaume ajiepushe na dhahabu zote. Dhahabu anaivaa anayehitajia uzuri na kujipamba, kama mwanamke. Anavaa ili ampambie mume wake ili avutikiwe naye. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
أَوَمَن يُنَشَّأُ فِي الْحِلْيَةِ وَهُوَ فِي الْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ
“Hivi kweli yule aliyelelewa katika mapambo naye katika mabishano si mbainifu.” (43:18)
Wanawake wanahitajia dhahabu ili kuwapambia waume. Mwanaume hahitajii hilo. Mwanaume anapambiwa nawala hajipambi kwa ajili ya mwingine. Isipokuwa baina yake yeye na mke wake kwa kila mmoja kumpambia mwenzake kutokana na mshikamano unaopatikana kwa kufanya hivo.
Lakini pasina kujali lengo wala hali yoyote ile haijuzu kwa mwanaume kuvaa dhahabu. Lakini kuvaa fedha ni sawa. Inajuzu kwa mwanaume kuvaa pete ya fedha. Lakini kwa sharti katika kufanya hivo kusiwepo imani fulani kama wanavofanya baadhi ya watu wanapowaiga manaswara katika kuvaa pete ya ndoa kati ya wanandoa.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (2/444-445)
Imechapishwa: 21/08/2025
https://firqatunnajia.com/haijuzu-kwa-mwanaume-kuvaa-vitu-vya-dhahabu/