36 – Dhikr ni nuru kwa mwenye kuitaja ulimwenguni, ni nuru kwake ndani ya kaburi lake na ni nuru kwake kesho Aakhirah. Nuru hiyo itamwangazia Njia mbele yake. Hakuna kitu kinachotia nuru nyoyo na makaburi kama kumtaja Allaah (Ta´ala). Amesema (Ta´ala):
أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَاَ
“Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamuhuisha na tukamjaalia nuru anatembea kwayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yuko katika viza si mwenye kutoka humo?”[1]
Wa mwanzo ni muumini aliyepata mwangaza kwa imani juu ya Allaah, kumpenda, kumjua na kumtaja. Wa pili ni mwenye kughafilika na Allaah (Ta´ala), aliyekengeuka na kumtaja Yeye na kumpenda. Suala lote linahusiana na na nuru. Mafanikio yote yanahusiana na nuru. Mashaka yote yanahusiana na kuikosa nuru hiyo. Kwa sababu hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisisitiza mno katika kumuomba Mola wake (Tabaarak wa Ta´ala) kumfanya kuwa nuru katika nyama zake, mifupa yake, mishipa yake, nywele zake, ngozi yake, usikivu wake, kuona kwake, juu yake, chini yake, kulia kwake, kushoto kwake, nyuma yake na mbele yake mpaka anafikia kusema:
“Na nifanye mimi kuwa nuru.”[2]
Akamwomba Mola wake (Tabaarak wa Ta´ala) amfanye kuwa nuru katika kila chembe ya mwili wake wa nje na wa ndani, amfanye amezungukwa na nuru kutoka kila upande na amfanye yeye mzima kuwa nuru. Dini ya Allaah (´Azza wa Jall) ni nuru. Kitabu Chake ni nuru. Mtume Wake ni nuru. Nyumba aliyowaandalia waja Wake ni nuru inayong’aa. Yeye Mwenyewe (Tabaarak wa Ta´ala) ni nuru ya mbingu na ardhi. Miongoni mwa majina Yake ni nuru. Giza limeangazwa na nuru ya uso Wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema siku ya Twaaif:
اعوذ بنور وجهك الذي أشرقت له الظلمات وصلح عليه أمر الدنيا والآخرة.أن يحل على غضبك، أو ينزل بي سخطك.لك العتبى حتى ترضى ولا حول ولا قوة الا بك
“Ninajilinda kwa nuru ya uso Wako ambayo kwayo giza liliangaziwa, yakatengemaa kwayo mambo ya dunia na Aakhirah kwamba nikapatwa na ghadhabu Yako au nikashukiwa na hasira Yako. Ninakupendeza mpaka uridhike. Hapana nguvu wala namna isipokuwa kwa msaada Wako.”[3]
Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Hakuna usiku wala mchana kwa Mola wenu. Nuru ya mbingu ni kutoka katika nuru ya uso Wake.”[4]
Ameipokea ´Uthmaan ad-Daarimiy.
[1] 6:122
[2] al-Bukhaariy (6316) na Muslim (763).
[3] at-Twabaraaniy katika “ad-Du´aa’” (2/1280).
[4] ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah (90) ya Ibn Mandah. Imethibiti kwa mujibu wa Ibn Taymiyyah katika “Majmuu´-ul-Fataawaa” (6/364).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 114-116
- Imechapishwa: 21/08/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 114-116
Imechapishwa: 21/08/2025
https://firqatunnajia.com/63-njia-bora-ya-kuangaza-maisha-yako/