Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

“Murji-ah hawaingii ndani ya Bid´ah hizi kubwakubwa. Wanazuoni wengi na wafanya ´ibaadah wameingia ndani ya fikira zao. Waliendelea kuzingatiwa kuwa katika Ahl-us-Sunnah mpaka pale ambapo watapindukia na fikira zao kuwa kali zaidi.”[1]

Maneno yake Shaykh-ul-Islaam yanafahamisha yafuatayo:

1 – Irjaa´ sio katika Bid´ah kali. Udhahiri ni kuwa anawakusudia Murji-ah al-Fuqahaa´ na sio wale Murji-ah waliopindukia kama vile Jahmiyyah na Karraamiyyah.

2 – Wale Ahl-us-Sunnah waliotangulia walikuwa wakiwazingatia Murji-ah al-Fuqahaa´ kuwa katika Ahl-us-Sunnah mpaka pale wanapopindukia.

Wanasemaje juu ya hilo wale Haddaadiyyah wapya na khaswa katika kilele chao Fawziy al-Bahrayniy? Je, watamtukana Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah kama ambavo mwalimu wao Mahmuud al-Haddaad alivyokuwa akimtukana kwa kusema:

1 – Anachukulia wepesi suala la Irjaa´.

2 – Ameenda kinyume na maafikiano ya Ahl-us-Sunnah aliposema kuwa Bid´ah ya Murji-ah al-Fuqahaa´ inahusiana na matamshi peke yake.

3 – Amemtuhumu Shaykh-ul-Islaam uwongo pale aliposema:

“Miongoni mwa maoni hayo ni kwamba Murji-ah al-Fuqahaa´ ni katika Ahl-us-Sunnah. Tahadhari na uwongo!”

4 – al-Haddaad amesema:

“Kwa mujibu wa Murji-ah ni kwamba waislamu wote wako katika kiwango kimoja cha imani kama vile Jibriyl. Wanaona kuwa ni kufuru imani kupanda na kushuka. Aidha wanasema kuwa matendo sio katika imani. Baada ya yote haya wako wanaosema kuwa magomvi ni Bid´ah ya kimatamshi na si ya kihakika. Endapo tutalikubali hilo, basi amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Akukose mama yako! Kuna kitachowarusha watu Motoni kama sio kwa ajili ya ndimi zao?”

Hapa anamkusudia Shaykh-ul-Islaam. Halafu akasema:

“Baada ya haya eti wanaitwa “Murji-ah wa Ahl-us-Sunnah”. Kusemwe nini baada ya haya? Jahmiyyah wa Ahl-us-Sunnah? Murji-ah ni kipote kimoja[2] kilicho nje ya Ahl-us-Sunnah. Ni vipi watakuwa miongoni mwao?”[3]

Unaona jinsi anavyomwandama Shaykh-ul-Islaam kila pale anapopata fursa ya kumtukana kwa mbinu hii ya vitimbi. Je, anawakusudia Murji-ah pale anapomzungumzia mwenye kusema kuwa magomvi ni ya kimatamshi na si ya kihakika? Katika zile nukuu zilizotangulia Shaykh-ul-Islaam mwenyewe amebainisha ni kina nani anaowakusudia. Tazama malazimisho yake ya batili na kusema:

“Kusemwe nini baada ya haya? Jahmiyyah wa Ahl-us-Sunnah?”

Je, Irjaa´ ni kama ´Aqiydah ya Jahmiyyah? Je, Ibn Taymiyyah anawaona Murji-ah al-Fuqahaa´ ni sawa na Murji-ah waliochupa mipaka au Jahmiyyah? Je, akemewe Ahmad na Salaf waliosalia kwa sababu ya kuwachukulia wepesi Murji-ah al-Fuqahaa´ wasiokuwa walinganizi? Nimeraddi matusi ya al-Haddaad ya kiovu dhidi ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah kwa kina kabisa[4].

Matusi haya ya khatari ya al-Haddaad dhidi ya Shaykh-ul-Islaam chimbuko lake ni wale Haddaadiyyah wapya, akiwemo Fawziy al-Bayrayniy, wanaotumia fursa dhidi ya Ahl-us-Sunnah. Msingi huo ni kumtia ndani ya Bid´ah yule mwenye kusema kuwa makinzano kati ya Ahl-us-Sunnah na Murji-ah al-Fuqahaa´ ni ya kimatamshi tu. Bali wanamwingiza ndani hata yule ambaye haonelei hivo, kama vile mimi, ili wapate kumfanyia Tabdiy´ na kumpiga vita.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (3/357).

[2] Ni uwongo. Murji-ah ni mapote mengi na wanatofautiana. Bwana huyu yeye amewafanya wote ni pote moja ili apate kuwaponda Ahl-us-Sunnah kwa jumla na khaswa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah.

[3] Yawma laa Dhwilla illaa Dhwilluh, uk. 70

[4] Tazama ”Twa´n al-Haddaad fiy ´Ulamaa’-il-Islaam”, uk. 2-7

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 201-203
  • Imechapishwa: 08/08/2023