03. Fadhilah za subira ndani ya Qur-aan

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ

“Bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao [katika kazi zenu]. Wabashirie wale wenye kusubiri ambao unapowafika msiba basi husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea – hao zitakuwa juu yao baraka kutoka kwa Mola wao na rehema na hao ndio wenye kuongoka.”[1]

وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ

“Tafuteni msaada kupitia subira na swalah, kwani hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa wanyenyekevu.”[2]

وَاللَّـهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ

”Na Allaah anawapenda wenye subira.”[3]

إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ

“Hakika si venginevyo wale wenye kusubiri watalipwa kikamilifu ujira wao pasi na hesabu.”[4]

Imesemekana kuwa watalipwa thawabu nyingi kiasi cha kwamba hawatoweza kuzihesabu wala kuzidhibiti. Aayah tukufu zinazotaja subira na thawabu zake ni nyingi.

[1] 2:155-157

[2] 2:45

[3] 3:146

[4] 39:10

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdillaah bin Naaswir-id-Diyn ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bard-ul-Akbaad ´inda Faqd-il-Awlaad, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 08/08/2023