Kwa ajili hiyo nasema:

Ametakasika na mapungufu Yule anayewajaribu watu

Anaowapenda – mtihani ni zawadi

Subiri kwa mtihani na kuwa ni mwenye kuridhia

hiyo ndio dawa

Jisalimishe kwa Allaah yale aliyohukumu –

na Allaah anayafanya ayatakayo

Tanzia ni Sunnah kubwa na ni sifa inayopendeza na inayoridhiwa. Sijaona tanzia ilio kubwa zaidi kwa aliyefikwa na msiba kuliko Kitabu kilicho na Aayah za Qur-aan kilichoambatana na khabari, maneno, simulizi na mashairi. Kwa ajili hiyo nikakusanya yale niliyowahi na vyanzo na uanishaji uliyotajwa, kwenda kwa yule anayelengwa na kila ambaye amefikwa na msiba iwe ni faraja na uokozi, pia nishirikiane na aliyefikwa na msiba katika thawabu na wema wake. ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kumpa rambirambi aliyefikwa na msiba, basi anapata mfano wa ujira wake.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy, Ibn Maajah na wengineo.

 ´Amr bin Hamz (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakuna muumini yeyote anayempa pole ndugu yake kutokana na msiba uliyompata isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall) humvisha vazi la heshima siku ya Qiyaamah.”[2]

Ameipokea Ibn Maajah.

Kumepokelewa mfano wa hayo kutoka kwa Abu Hurayrah, Abu Barzah al-Aslamiy, Jaabir na wengineo (Radhiya Allaahu ´anhum).

[1] at-Tirmidhiy (1073) na Ibn Maajah (1602). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf at-Tirmidhiy” (1073).

[2] Ibn Maajah (1601). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (1311).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdillaah bin Naaswir-id-Diyn ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bard-ul-Akbaad ´inda Faqd-il-Awlaad, uk. 28-30
  • Imechapishwa: 08/08/2023