Swali: Kama kuna mtu ana elimu ndogo na katika mji wake kuna maovu na Bid´ah zilizoenea. Mtu huyu asubiri mpaka amalize masomo yake na awe na uelewa wa Dini zaidi halafu ndio afunze au akimbilie kufunza yale anayoyajua?

Jibu: Afunze kwa kiasi cha anavyojua. Afunze kwa kiasi cha anavyojua. Mwenye kujifunza kitu awafunze wengine hata kama itakuwa ni kidogo. Anachotakiwa ni kuwafunza nacho wengine hata kama kitakuwa kidogo. Asisubiri mpaka amalize masomo yake au mpaka awe mwanachuoni. Aende daraja kwa daraja. Maovu yanazidiana. Aanze [kukataza] kitu ambacho ni muhimu zaidi kuliko kingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14897
  • Imechapishwa: 21/04/2015