Funguo zilizopotea zilizoning´inizwa msikitini

Swali: Kuning´iniza funguo zinazookotwa maeneo ya nyuma ya msikiti kunaingia katika matangazo yaliyokatazwa?

Jibu: Sio kutangaza. Ima akaziacha funguo hizo mahali zilipodondoka msikitini ili mwenye nazo aje kuzichukua au azipandishe juu ya kitu na aziweke mahali kunapoonekana. Matangazo yanakuwa kwa kuzungumza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 27/02/2022