Swali: Inatokea wakati mwingine baadhi ya wanafunzi wanaacha vitabu vyao msikitini kwa kipindi kirefu na hawatambuliki wenye navyo. Imamu wa msikiti avifanye nini? Je, aviuze na atumie thamani yake kwa ajili ya msikiti?

Jibu: Hapana, asiviuze. Ikiwa anamjua mmiliki wake, basi amwite na kumwambia akichukue. Kama hamjui mmiliki wake, basi kitabu kinakuwa na hukumu ya waqf; kibaki msikitini na kitatumiwa na yule anayetaka kukisoma. Njia nyingine ni kwamba kinaweza kupelekwa katika maktabah ya ummah ambapo kila mmoja anaweza kufaidika nacho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 27/02/2022